Nini tunajifunza kwenye teuzi za wagombea wa u Rais -2020?

 • Inawezekana ACT Wazalendo wakaonekana ni chama kidogo kisiasa lakini kwa muda mfupi tangia Maalim Seif na kundi lake kuingia ACT Wazalendo wakitokea CUF wamebadilisha kabisa mtazamo na vision ya hiki chama

  • Suala la Membe kujiunga na ACT Wazalendo linaonekana limefanywa kimkakati sana na kufanyiwa uchambuzi kwa muda MREFU sana
  • Uchaguzi wa mgombea mwenza wa Membe umeonyesha jinsi gani ACT Wazalendo hawana mzaha wnapokwenda kushiriki uchaguzi mkuu wa Oktoba 2020
  • Hotuba ya Membe kukubali uteuzi wa chama chake kukubali kuwa mgombea umeakisi mtazamo wa chama halisi cha upinzani kinachojiandaa kuleta ushindani wa kweli kwenye uchaguzi wa Oktoba.Hotuba ya Membe imesheheni mambo kedekede anayofikiria na kutamani kuyafanya atakaposhinda uchaguzi tena kiuhalisia kabisa na siyo porojo.
  • ACT Wazalendo kimejionyesha kuwa kiko tayari kufanya siasa za kiushindani  wa hoja na kwa kutumia takwimu na uhalisia wa nini hakiko sawa na nini watafanya sawa wakiingia madarakani.
  • Kwa mtazamo wangu wa haraka haraka ACT Wazalendo walijipanga sana kushiriki huu uchaguzi kuliko wakati mwingine wowote.