Corona yapiga hodi ofisi ya Waziri Mkuu -Dodoma

 • Taarifa toka ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu yuko Dodoma zinasema kuwa mwanzoni mwa wiki wiki hii mmoja wa madereva wa Waziri Mkuu na mlinzi wa TISS wamekufa kwa dalili za corona.

  Chanzo chetu cha habari kimeendelea kusema dereva huyo na mlinzi huyo walikuwa kwenye msafarsa wa Waziri Mkuu walipokuwa Masasi kwenye mazishi ya Mkapa. 

  Hali ni ya taharuki sana ndani ya ofisi ya Waziri Mkuu kufuatia vifo hivi na wanafanyakazi wanaogopa kuvaa barakoa kwa kuna Rais Magufuli hataki kuona mtu yoyote hasa akiwa ni mfanyakazi wa serikali anavaa barakoa kwa kuna ameshaitangazia dunia kuna maombi yameondoa corona nchini.maombi ambayo ni Tanzania pelée ndiyo wanayajua lakini nchi zingine duniani hawayajui kabisa..

  dichuatanzania inawapo pole wafiwa lakini inawahimiza watanzania muendelee kuchukua tahadhali kwa kuwa corona ipo na inaendelea kuuwa kila siku na ukweli huo serikali inaujua.

1 comment
 • Brown Scorpion
  Brown Scorpion Na bado wanajiandaa kwerenda kwenye kampeni.. Tutapata tu tunachokitaka kama nchi maana tumechagua kuwa wajinga na wapumbavu kwa kufuata maneno ya watawala wasiofikiria na kuonea huruma maisha ya watanzania..
  August 6, 2020 - Report