DC KASESELA NI MFANO HALISI WA VIONGOZI WA UTAWALA WA MAGUFULI

  • Leo tumeona kwenye mitandao ya kijamii jinsi ambavyo DC Kasesela anasimama mbele ya kadamanasi ya kutusi watu bila kuwa na uoga wowote. Najiuliza huu umekuwa ni utaratibu wa utawala wa awamu hii? Mtu mwenye dhamana ya mkuu wa wilaya ambaye ni muwakilishi wa Rais kwenye wilaya husika anawezaje kutamka kwa mwananchi kuwa " kalisha matako weweee" tena anaiongea kauli hiyo kwa kuirudia rudia zaid i ya mara tatu.

    Sijashangaa sana kwa kuwa Magufuli akiwa Rais enzi za uhai wake alishawahi kuwaambia wananchi"bakini na mavi yenu nyumbani" hiyo ni kauli ya Rais wa nchi kwenda kwa mwananchi aliyeuliza swali. 

    Tumeshuhudiwa wakuu wa wilaya na viongozi wengine wanachapa viboko wananchi hadharani kwa kuwa wao ni viongozi na wamepewa dhamani ya kuongoza basi wanadhani wana mamlaka ya kufanya lolote juu ya yoyote yule..

    Hali hii imefika hapa kwa kuwa ndani ya serikali hakuna adabu na nidhamu katika kufanya utumishi wa umma na hili limekuwa wazi karibu maeneo mengi sana..Kama nchi kuna mahali Tanzania inatakiwa ijitafakari upya..