Tanzania yalipa faini kuzuia ndege kukamatwa

  • Tanzania imekuwa nchi ya ajabu sana. Yaani nchi inalipa fidia kimya kimya na bila hata bunge kujua na fedha zinatoka. Hivi tumekuwa nchi ya aina gani mambo haina vyombo vinavyoangalia haya mambo? Mpaka lini katiba ya Tanzania itaendelea kudharauliwa na kutoheshimiwa? 

    Kwa nini serikali inajiona yeynyewe ndiyo final na inaweza kufanya kila kitu wanachotaka ili mradi tu wao ni serikali? Maamuzi ya hovyo ya serikali ndiyo yanapelekea kufunguliwa hizi kesi kila kukicha na wanaolipa ni walipa kodi wa nchi hii. 

    Hizi fedha ni kodi za wananchi ambazo serikali haijali wala kuheshimu wanafanya makosa na wakikutwa na shida wanalipa faini na tena wanakwenda mbali zaidi wanaidhinisha malipo bila hata kuomba approval ya bunge..

    Bila kuwa na katiba mpya ndani ya Tanzania uozo wa aina hii hautakaa uishe milele