Ofisi za Chadema kanda ya Kaskazini zachomwa moto

  • Habari zilizotufikia ni kuwa ofisi za Chadema Kanda ya Kaskazini zimechomwa moto usiku wa kuamkia leo. Ikumbukwe mgombea urais kwa ticket ya Chadema Mh Lissu leo anaanza ziara kanda ya kasakazini kutafuta wadhamini. 

    Napata shida sana kuamini watu waliofanya siasa miaka zaidi ya minne peke yao wanajawa na hofu ya kiasi hiki kabla hata ya kampeni hazijaanza? Hivi kampeni zikianza CCM wataweza kuhimili kwenye miezi miwili ya kampeni? Kama hali ya sasa ni hii na mnaonekana wazi mmejwa hofu hivi kweli mtafika salama Oktoba 2020?

    Kama hii nchi itatumbukia kwenye machafuko basi tunajua kabisa CCM na vyombo vya dola vya dola wako nyuma ya matukio haya ya kishenzi na yasiyo ya kistaarabu..