Forums » Tanzania Covid-19 DASHBOARD

Tahadhari dhidi ya corona kuelekea kampeni za uchaguzi

 • August 13, 2020 6:05 PM MSK

  Chanzo chetu cha habari ndani ya wizara ya afya kinasema kwa takwimu walizonazo mpaka sasa ni kuwa idadi ya vifo inazidi kuongezeka kila siku hasa kwa Zanzibar 

  Ni vyema watanzania na hasa wanasiasa wakaelewa kuwa ni jambo la busara sana na lenye kujali kama watachukua tahadhari kuelekea kwenye mikusanyiko wakati wa kampeni za uchaguzi zinazoanza hivi karibuni..

  Corona bado ipo sana na watu wanaangamia lakini kwa kuwa Serikali imeamua kuaminisha watu kuwa maombi yamesaidia corona imeisha, basi ni vyema kuchukua tahadhari. Tumeshuhudia mikusanyiko mikubwa sana kwenye hekaheka za kutafuta wadhamini kwa wagombea wa uRais wa ACT Wazalendo na Chadema.

  Viongozi wetu wa wameamua kututoa sadaka ndiyo maana hawajali na hawataki kujali,kama ilivyo kwa waziri mkuu Majaliwa ndani ya ofisi wake kafa dereva wake na mlinzi wake ndani ya masaa 15 toka wamerudi Masasi kwenye mazisi ya hayati Mkapa. Hawajali kabisa!

 • October 20, 2020 4:02 PM MSK
  1